Get Up to 0% to 25% OFF Ordered Bibles* Accondingly.

Membership

Membership

TSh
 
Select Payment Method
ipayflutterwave
Personal Info


Customer Info Powered by Flutterwave: Accepts Mastercard, Visa, Verve, Discover, AMEX, Diners Club and Union Pay.

Donation Total: TSh 15,000.00

Uanachama

Chama cha Biblia cha Tanzania kinapokea Wakristo wote bila kujali ujinsia, rangi, utaifa, lugha, kazi au biashara, ambao kwa hiyari yao wapo tayari kufuata na kujihusisha na Malengo na Madhumuni ya Chama.

Chama kina na aina zifuatazo za uanachama:

  1. Uanachama wa Kikundi
  2. Uanachama wa Maisha
  3. Uanachama wa Pamoja wa Maisha (mme na mke)
  4. Uanachama Kamili wa kila Mwaka
  5. Uanachama wa Ushiriki
  6. Uanachama wa Heshima
  7. Uanachama wa Klabu ya Biblia kwa Mwezi

“Uanachama wa Kikundi”: Kanisa lolote la mahali, usharika, shirika au taasisi, ambao hutumia Biblia kama msingi wa imani yao na ambao hutoa michango ya kila mwaka, kama itakavhyokuwa inapangwa mara kwa mara na Bodi, wataweza kuwa wanachama wa kikundi kwa mwaka ule wanaolipa mchango wa uanachama, na wakishaandikishwa, watakuwa na haki ya kutuma mwakilishi kuhiriki katika Mkutano Mkuu wa Mwaka na pia katika mikutano ya ngazi za Matawi na watakuwa na haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.

“Uanachama wa Maisha”: Mtu yeyote anayekiunga mkono Chama na anayependa kuwa

Mwanachama wa Maisha anaweza, baada ya kulipa kiingilio na mchango wa uanachama wa Maisha kama itakavyokuwa inapangwa mara kwa mara na Bodi ya Wakurugenzi, atakuwa mwanachama wa maisha na atakuwa na haki ya kupiga kura katika Mkutano wa Tawi na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Taifa.

“Uanachama wa Pamoja wa Maisha”: Wanandoa wowote baada ya kulipa mchango kama

utakavyokuwa unapangwa na Bodi ya Wakurugenzi mara kwa mara watakuwa Wanachama wa Maisha wa Chama. Wanachama wa aina hii kila mmoja wao atakuwa haki ya kupiga kura.

“Uanachma Kamili wa Mwaka”: Mtu yeyote anayekiunga mkono Chama anaweza kuwa

Mwanachama Kamili wa Mwaka kwa kulipa kiingilio na mchango wa mwaka kama itakavyokuwa inapangwa mara kwa mara na Bodi ya Wakurugenzi. Wanachama Kamili waliolipa michango yao watakuwa na haki ya kupiga kura katika Mikutano ya Matawi na Mkutano Mkuu wa Kitaifa kwa mwaka waliolipia.

“Uanachama wa Kushirikishwa”: Mtu yeyote aliye chini ya miaka 18, baada ya kujiandikisha

au kuandikishwa, anaweza kuwa Mwanachama wa Kushirikishwa katika mwaka ambao amelipia mchango wa uanachama wa kushirikishwa. Wanachama wa Kushirikishwa wanaweza kuhudhuria Mikutano Mkikuu ya Chama, lakini hawatakuwa na haki ya kupiga kura.  

“Uanachama wa Heshima”: Bodi ya Wakurugenzi itakuwa na mamlaka ya kumteua

Mwanachama wa Heshima miongoni mwa watu wale ambao wametoa mchango wa kipekee kwa Chama. Wanachama wa aina hii wanaweza kuhudhuria mikutano, lakini hawatakuwa na haki ya kupiga kura.

“Uanachama wa Klabu ya Biblia kwa Mwezi:” Utakuwa wazi kwa mtu yeyote na anaweza

kuwa mwanachama wa aina nyingine wa Chama kama ilivyoainishwa katika Katiba hii, ambaye baada ya kujiandikisha anajitolea kutoa michango kila mwezi kama atakavyoahidi. Mwanachama wa Klabu ya Biblia kwa Mwezi ambaye hayumo katika aina nyingine ya uanachama anaweza kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama lakini hatakuwa na haki ya kupiga kura.

[]
× How can we help you?