Get Up to 0% to 25% OFF Ordered Bibles* Accondingly.

MCHANGO WA KILA MWEZI

TSh
 
Personal Info

Billing Details

Please follow the following instructions if you are paying with M-PESA

Step 1: *150*00# press ok
Step 2: Pay by M-Pesa (Lipa kwa M-PESA) 4
Step 3: Enter busines number (Ingiza namba ya kampuni) 4
Step 4: Enter business number (namba ya kampuni ni) is 890890

Step 5: Enter Reference Number (Weka Nambari ya Marejeleo) eg. ADA, BIBLE-MONTH, WATOTO

Step 6: Enter you PIN (Andika Neno lako la Siri)

Step 7: Press 1 to accept and make sure the name is The Bible Society of Tanzania

Donation Total: TSh 280,000.00

Changia Biblia ya bure kwa magereza nchini Tanzania  

Wafungwa huwa wanamuda mwingi wa ziada ambao unaweza kutumika vibaya kama usipotumika kwenye shughuli zenye tija. Mradi huu unalenga kuwapatia wafungwa Biblia bila malipo ili kuwawezesha kupata Neno la Mungu. Jambo hili litawawezesha wafungwa kusoma Biblia katika muda wao wa mapumziko hivyo kufahamu na Neno la Mungu na kukutana na Bwana Yesu Kristo alie faraja na Rehema nyingi wa wanadamu wote hapa duniani.

Mpango huu muhimu utakuwa wa miaka mitatu na unalenga kuwafikia wafungwa 25,000. Biblia moja inaweza kutumika kwa pamoja na wafungwa hadi watano.

Tunatarajia kwamba mradi huu utakuwa na matokeo makubwa kwa wafungwa katika kuwabadilisha tabia, kuwapa tumaini na kuwafanya wawe raia wawajibikaji pindi watakapomaliza vifungo vyao na kurudi kwenye jamii.

Mabadiliko ya tabia huanza pindi wakiwa bado wafungwa. Uzoefu unaonesha wale waliompokea Yesu magelezani ni mfano wa kuigwa na hawana usumbufu kwa wafungwa wenzao na mamlaka za magereza.

Tunakuomba wewe mdau, mwanachama na mtu mwenye mapenzi mema ungana nasi katika kuchangia Biblia kwa kadili ya unavyoweza ili kuwafikia wafungwa wengi katika magereza yao hapa nchini.

Chama cha Biblia cha Tanzania kushirikiana na wadau kitatoa Biblia 5000 za bure kwa wafungwa Tanzania. 

Jinsi mradi/mpango huu utakavyowasaidia walengwa (wafungwa)

1. Kutakuwa na mabadiliko mazuri ya tabia kati ya wafungwa.

2. Kupunguza machafuko katika magereza.

3. Wafungwa watapata mwelekeo  wa maisha yao wakati wakiwa gerezani na hata baada ya kutoka gerezani.

4. Utasaidia wafungwa kuwa na amani ya akili hasa wale wanaotumikia fungo vya muda mrefu.

Mwenyezi Mungu na akubariki sana katika kuungana nasi katika kuchangia mpango huu muhimu kwa jamii yetu na Taifa kiujumla.

This post is also available in: swahili