Error: This donation form has no available payment methods. Please try your donation again later.
Mnunulie mtoto Biblia!”
Mwezeshe mtoto wa Tanzania kulijua neno la Mungu. (Mathayo 19:14).
Chama cha Biblia cha Tanzania kina jukumu la kuhakiksha neno la Mungu linawafikia watu wote popote pale walipo katika lugha ambayo wanaielewa na kwa bei wanayoimudu. Watoto ni kundi ambalo linahitaji kufikiwa pia ili kuwezesha kizazi cha kesho kuwa na msingi wa imani.
Chama cha Biblia cha Tanzania kimeandaa na kimekuwa kikitoa maandiko mbalimbali kwa ajili ya watoto, matarajio na maombi ya Chama cha Biblia ni kuona watoto wengi wanafikiwa na Neno la Mungu.
Tunaamini, mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu ndani ya familia,jamii na kanisa kwa ujumla. Ni wajibu wa mzazi/mlezi kumpa mtoto chakula hadi anapokuwa mkubwa ndipo wajibu huo unakuwa wa mtoto. Ndivyo ilivyo kwenye mambo ya kiroho, Neno la Mungu linamtaka mzazi /mlezi kumlea mtoto kiroho tangia akiwa mdogo ili baada ya muda jukumu hilo lirudi kwa mtoto mwenyewe anapokuwa mkubwa. Ili kuweza kufanikiwa katika hili mzazi/mlezi anapaswa kumfundisha mtoto wake neno la Mungu. (Mith.22:6)
Ni wajibu wa wazazi kujitoa nafsi zao kuwafundisha mambo ya kimungu pamoja na adabu njema. Mafundisho ya kikristo yana makusudi ya kumjengea mtoto ama watoto msingi wa imani na kuwafanya wajitenge mbali na mambo maovu; hivyo kuwa katika mwenendo wa kumcha Mungu.
Wazazi wanapaswa kuwaonyesha njia watoto wao jinsi ya kumtafuta Mungu wao wenyewe ili kuwafanya wafurahie mambo halisi ya kiroho ambayo Mungu anawatendea; hawataweza kuyasahau kabisa hata wajapo kuwa wakubwa au watu wazima. “Naye hataiacha”. Kwa kanuni hii, mtoto aliyefundishwa Neno la Mungu na wazazi wake hawezi kuziacha njia alizoelekezwa.
Chama cha Biblia cha Tanzania kina lengo la kutoa Biblia 5000 za bure kwa watoto nchini Tanzania. Hivyo tunakuomba wewe mwenye mapenzi mema kuungana nasi kwa kutoa mchango wako wa upendo.
Msaada huu utawasaidia watoto kama ifuatavyo:-
- Kutakuwa na mabadiliko mazuri ya tabia kati ya watoto.
- Kupunguza machafuko katika watoto.
- Watoto watapata uongozi bora wa kimaadili wakati wangali watoto hata watakapokuwa wazee.
- Itasaidia watoto kuwa na amani ya akili hasa wale yatima.
Mwenyezi Mungu na akubariki sana unapoungana nasi katika mpango huu muhimu kwa watoto wa hapa nchini.
This post is also available in:
swahili